Joao afungua mlango Atletico

Mtanzania
Published: Dec 08, 2021 08:17:30 EAT   |  Sports

MADRID, Hispania MSHAMBULIAJI wa Atletico Madrid, Joao Felix, atafungasha kila kilicho chake na kutimka klabuni hapo mara tu usajili wa Januari, mwaka huu. Kwa mujibu wa taarifa, Mreno huyo mwenye umri wa miaka 22 ameshamwambia wakala wake amtafutie klabu ya kwenda. Ni katika hatua hiyo, ikaibuka kuwa Barcelona wanamtazama kwa jicho la karibu mchezaji huyo […]

MADRID, Hispania

MSHAMBULIAJI wa Atletico Madrid, Joao Felix, atafungasha kila kilicho chake na kutimka klabuni hapo mara tu usajili wa Januari, mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa, Mreno huyo mwenye umri wa miaka 22 ameshamwambia wakala wake amtafutie klabu ya kwenda.

Ni katika hatua hiyo, ikaibuka kuwa Barcelona wanamtazama kwa jicho la karibu mchezaji huyo wa zamani wa Benfica.

Katika nyakati tofauti, jina la Joao limewahi kuhusishwa na klabu mbalimbali, ikiwamo Liverpool.