Huyu ndiye kocha mpya Man City

Mtanzania
Published: Dec 08, 2021 08:14:16 EAT   |  Sports

AMSTERDAM, Uholanzi MABOSI wa Manchester City wanataka kocha wa Ajax, Erik ten Hag, atue kwao endapo Pep Guardiola ataondoka hapo baadaye. Guardiola, ambaye amekuwa akiinoa Man City tangu mwaka 2016, inasemekana anataka kutimka atakapomaliza mkataba wake Juni, 2023. Hayo ya Man City yanakuja huku ikifahamika kuwa Ten Hag anahusishwa pia na Manchester United wanaotaka akali […]

AMSTERDAM, Uholanzi

MABOSI wa Manchester City wanataka kocha wa Ajax, Erik ten Hag, atue kwao endapo Pep Guardiola ataondoka hapo baadaye.

Guardiola, ambaye amekuwa akiinoa Man City tangu mwaka 2016, inasemekana anataka kutimka atakapomaliza mkataba wake Juni, 2023.

Hayo ya Man City yanakuja huku ikifahamika kuwa Ten Hag anahusishwa pia na Manchester United wanaotaka akali kiti cha kocha wa muda, Ralf Rangnick.

Aidha, zipo taarifa zinazodai kuwa Mholanzi mwenye umri wa miaka 51 anavutiwa zaidi na ofa ya kwenda Old Trafford na si Etihad.