Halotel yaipiga tafu Sekondari ya Bangulo

Mtanzania
Published: Oct 20, 2022 14:22:59 EAT   |  Educational

Na Imani Nathaniel, Dar es es Salaam Kampuni ya simu za mkononi ya Halotel imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya masomo vya zaidi ya Sh milioni 10 kwa walimu na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Bangulo iliyoko jijini Dar es Salaam. Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Oktoba 20, 2022 Mkuu wa Kitengo cha […]

Na Imani Nathaniel, Dar es es Salaam

Kampuni ya simu za mkononi ya Halotel imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vya masomo vya zaidi ya Sh milioni 10 kwa walimu na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Bangulo iliyoko jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Oktoba 20, 2022 Mkuu wa Kitengo cha bidhaa na mawasiliano wa kampuni hiyo, Sakina Makabu, amesema mpango huo ni kuunga mkono juhudi za Serikali ambazo ni kuhakikisha shule zote nchini zinapata mahitaji na vifaa mhimu ili kuboresha kiwango cha elimu nchini.

“Halotel tumeamua kutoa msaada wa vifaa ambavyo ni meza na viti vya waalimu, kabati la vitabu na mafaili, kompyuta tatu na printa, ikiwa ni moja wapo wa muitikio wa kampuni yetu katika kuboresha mazingira ya ufundishaji na kukuza ufaulu mashuleni,” amesema Sakina.

Aidha, Halotel inatoa huduma ya kimasomo ijulikanayo kama “Halostudy” ambavyo humuwezesha mwanafunzi kusoma mitaala mbalimbali kwa njia ya matandao, huku ikiwa na mpango mpya wa kuboresha sekta hii kidijitali kwa ngazi ya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini ambapo huduma hii kidijitali itamuwezesha mwanafunzi kuwekwa voucha yenye thamani ya Sh 1,500 kila mwezi.

Kwa upande wa Mkuu wa shule hiyo, Hessein Ramadhan, amesema kuwa ni faraja kupokea msaada kutoka Kampuni ya Halotel na tunawashukuru kwa kuendelea kuwa karibu na jamii kwa kuthamini Sekta ya Elimu nchini.

“Nina amini vifaa hivi vitasaidia walimu na wanafunzi huku nikimshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Samia Suluhu kwa kutujengea shule yetu ya sekondari ya Bangulo na ninawaomba wadau mbalimbali wajitokeze kuiga mfano wa kampuni ya Halotel,” amesema Ramadhani.

Naye Afisa Elimu wa Kata ya Pugu Stesheni, Gerald Kwinoma, ameishukuru kampuni ya Halotel kwa kutambua uhitaji wa Shule ya Sekondari ya Bangulo na kuleta vifaa vutakavyoinua viwango vya ufanisi katika masomo ya shule hii.

“Nawaomba huu usiwe mwisho katika kusaidia changamoto za elimu nchini na makampuni mbalimbali yakafanye kama mnavyofanya,” amesema Kwinoma.