Corona yaongeza vifo vya pombe Uingereza

Mtanzania
Published: Dec 08, 2021 09:47:49 EAT   |  News

LONDON, England KWA takwimu za mwaka jana, Uingereza imeshuhudia ongezeko kubwa la vifo vitokanavyo na ulevi wa pombe kwa kipindi chote cha janga la Corona. Katika hilo, wataalamu wa afya wametaja upweke uliotongana na watu kutakiwa kujitenga ulichagiza wengi wao kujiliwaza kwa pombe. Takwimu zimeonesha kuwa watu 8,974 walifariki kwa ulevi wa pombe mwaka jana, […]

LONDON, England

KWA takwimu za mwaka jana, Uingereza imeshuhudia ongezeko kubwa la vifo vitokanavyo na ulevi wa pombe kwa kipindi chote cha janga la Corona.

Katika hilo, wataalamu wa afya wametaja upweke uliotongana na watu kutakiwa kujitenga ulichagiza wengi wao kujiliwaza kwa pombe.

Takwimu zimeonesha kuwa watu 8,974 walifariki kwa ulevi wa pombe mwaka jana, likiwa ni ongezeko la asilimia 18.6 ukilinganisha na ilivyokuwa mwaka 2019.

Ukitazama takwimu hizo, unaona ni ongezeko kubwa zaidi kuwahi kutokea tangu mwaka 2001, kwa mujibu wa Ofisi ya Takwimu ya Uingereza.