Barca wamvutia kasi Ziyech

Mtanzania
Published: Dec 08, 2021 08:24:45 EAT   |  Sports

CATALUNYA, Hispania BARCELONA wamewasiliana na mabosi wa Chelsea wakiulizia saini ya kiungo wa kimataifa wa Morocco, Hakim Ziyech. Pia, inasemekana Barca wamezungumza na Chelsea juu ya kuipata saini ya mshambuliaji wa Kijerumani, Timo Werner. Kwa upande wake, kocha wa Chelsea, Thomas Tuchel, anaonekana kuwa tayari kuwaachia wachezaji hao waende Ligi Kuu ya Hispania (La Liga). […]

CATALUNYA, Hispania

BARCELONA wamewasiliana na mabosi wa Chelsea wakiulizia saini ya kiungo wa kimataifa wa Morocco, Hakim Ziyech.

Pia, inasemekana Barca wamezungumza na Chelsea juu ya kuipata saini ya mshambuliaji wa Kijerumani, Timo Werner.

Kwa upande wake, kocha wa Chelsea, Thomas Tuchel, anaonekana kuwa tayari kuwaachia wachezaji hao waende Ligi Kuu ya Hispania (La Liga).

Vilevile, Barca wanaamini wanaweza kuishawishi Manchester City ikubali kuwauzia mshambuliaji wao, Ferran Torres, kwa Pauni milioni 38.