Ajax wamtaka anayesota benchi Spurs

Mtanzania
Published: Dec 08, 2021 08:22:31 EAT   |  General

AMSTERDAM, Hispania KLABU ya Ajax inaangalia uwezekano wa kumsajili kiungo wa pembeni wa Tottenham, Steven Bergwijn. Mholanzi huyo anapitia kipindi kigumu tangu Antonio Conte awe kocha, ambapo amecheza dakika 13 tu, huku akiwa hajaanza hata mara moja. Bergwijn (24), hayuko peke yake kwenye majanga hayo kwani hata Dele Alli, Tanguy Ndombele na Joe Rodon nao […]

AMSTERDAM, Hispania

KLABU ya Ajax inaangalia uwezekano wa kumsajili kiungo wa pembeni wa Tottenham, Steven Bergwijn.

Mholanzi huyo anapitia kipindi kigumu tangu Antonio Conte awe kocha, ambapo amecheza dakika 13 tu, huku akiwa hajaanza hata mara moja.

Bergwijn (24), hayuko peke yake kwenye majanga hayo kwani hata Dele Alli, Tanguy Ndombele na Joe Rodon nao wamekalia kuti chini ya kocha huyo raia wa Italia.

Katika ofa yao, Ajax wameitaka Tottenham iwaruhusu wamchukue kwa mkopo Mholanzi mwenzao huyo kupitia usajili wa dirisha dogo, Januari, mwaka huu.