Simba yapewa wajeda, Yanga Kurugenzi, Azam Malimao

Mwanaspoti
Published: Nov 30, 2022 11:04:36 EAT   |  Sports

MABINGWA watetezi wa Kombe la Shirikisho Azam, Yanga imepangwa kucheza na Kurugenzi ya Simiyu inayoshiriki First League mchezo utakaochezwa uwanja wa Benjamin Mkapa. Droo ya hatua ya 64 za kombe hilo zimefanyika leo kwenye ofisi za Azam Media. Yanga ndio mabingwa watetezi wa kombe hilo wakiifunga Coastal Union msimu uliopita kwa mikwaju ya penalti 4-1 mchezo uliochezwa uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha. Upande wa Simba imepangwa kucheza na Eagle FC ambao ni wanashiriki Ligi ya Mabingwa wa mkoa mchezo utakaochezwa uwanja wa Benjamin Mkapa. Klabu zinazoshiriki Ligi Kuu zinakuwa nyumbani zikikutana na timu zinazoshiriki madaraja ya chini. Kombe la Shirikisho Azam lilirejea rasmi mwaka 2016 baada ya awali kusimamishwa kwa muda. Meneja wa mashindano TFF, Baraka Kizuguto amesema mechi hizo zitachezwa kwa kuangaliwa utaratibu wa kupishana viwanja visiweze kuingiliana. "Umeona tuna tarehe 9 na 11 kwahiyo kati ya hapo timu lazima zipishane kucheza, bingwa wa Mashindano haya ndio atakata tiketi ya kushiriki kimataifa,"amesema Kizuguto. Mechi hizo zinatarajiwa kuanza Disemba 9 mwaka huu hadi Disemba 11 na zitachezwa kwenye viwanja tofauti. RATIBA NZIMA ILIVYO Geita Gold vs Transit Camp (Nyankumbu, Geita) Ihefu vs Mtama Boy (Highland State) Kagera Sugar vs Buhare FC (Kaitaba) Dodoma Jiji vs TMA Stars (Jamhuri,Dodoma) Ruvu Shooting vs Ndanda (Uhuru) Namungo vs Kitayosce (Majaliwa) Polisi Tz vs Nyika FC (Ushirika) Mbeya City vs Stand Fc (Sokoine) Mtibwa Sugar vs TRA (Manungu) Prisons vs Misitu (Sokoine) Singida Bs vs Lipuli Fc (Liti) Coastal Union vs Tanga Middle (Mkwakwani) KMC VS Tunduru (Uhuru) Azam vs Malimao (Chamazi) Fountain Gate vs Rhino Rangers (Jamhuri, Dodoma) JKT Tanzania vs Biashara Utd (Mej G. Isamuhyo) Nduguti Stars vs Gwambina (Liti) African Lyon vs Mbuni (Uhuru) Kigoma Kwanza vs Buhaya (Lake Tanganyika) Cosmo Politana vs Mbeya Kwanza (Uhuru) Majimaji vs Ken Gold (Lake Tanganyika) Mashujaa vs Pamba (Lake Tanganyika) Polis Katavi vs Mbeya Road Mbao Fc vs Mapinduzi Fc (Nyamagana) Green Warriors vs Stand Utd (Mej G. Isamuhyo) Silent Ocean vs Copco (Uwanja utapangwa) Magereza DSM vs Pan African (Uhuru) E4M vs New Dundee (Samora) Afya FC vs African Sports (Uwanja utapangwa) Nzega vs KFC Fc