Mtanzania apewa fainali ya Al Ahly vs Wydad

Mwanaspoti
Published: May 31, 2023 08:11:55 EAT   |  Sports

Mjumbe wa kamati ya utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Alhaji Msafiri Ahmed Mgoyi ameteuliwa kuwa kamishna wa mechi ya kwanza ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Al Ahly na Wydad Casablanca, jijini Cairo, Misri, Juni 4. Uteuzi wa Mgoyi umekuja siku chache baada ya Mtanzania mwingine Baraka Kizuguto kusimamia mchezo wa pili wa nusu fainali ya mashindano hayo kati ya Mamelodi Sundowns na Wydad Casablanca katika majukumu ya mratibu wa mchezo. Taarifa iliyotolewa na TFF leo imeeleza kuwa Mgoyi ndiye amepewa jukumu hilo zito la kuwa bosi wa mechi hiyo ya fainali ya kwanza, inayokutanisha miamba hiyo miwili ya Kaskazini mwa Afrika. Kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo, Kamishna ndiye mwakilishi wa Rais wa CAF na ripoti yake ndio hutumika kwa asilimia nyingi kutoa uamuzi kuhusu mchezo husika. Mgoyi anakuwa mjumbe wa pili wa kamati ya utendaji ya TFF kupewa majukumu ya Ukamishna wa mechi msimu huu ambapo mwingine ni Khalid Abdallah