Mwanaspoti   
Mathare United kumpa Kimanzi msoto

Published: Nov 24, 2022 10:18:08 EAT   |  Sports

KOCHA wa zamani wa Harambee Stars, Francis Kimanzi, yupo tayari kuteuliwa tena kuwa mkufunzi wa Mathare United licha ya msoto mkali uliyopo klabuni humo kwasasa. “Kimanzi kaonekana akifanya mazoezi na wachezaji wa Mathare ila ni kwa kujitolea tu. Tayari mazungumzo baina yake na uongozi kumpa kazi yanaendelea. Kimanzi anaelewa vyema hali ngumu ya kifedha wanayopitia kwasasa Mathare ila yupo radhi kufanya kazi nao. Bado maamuzi hayajafikiwa ila kuna uwezekano mkubwa atakubali kazi,” chanzo kimoja kimeeleza. Kimanzi ni mchezaji wa zamani wa Mathare lakini pia ndiye kocha aliyewawezesha kutwaa ubingwa wao wa pekee Ligi Kuu Kenya mwaka 2008. Kutokana na historia hiyo na mapenzi yake kwa klabu, uongozi una matumaini kuwa hatawakataa licha ya hali ngumu ya kifedha wanayopitia kwasasa. Kimanzi hajakuwa na timu tangu alipochujwa na Wazito FC Januari mwaka huu. Mathare United waliyomaliza wa mwisho msimu uliyopita, walipata nafuu ya kurejea FKFPL baada ya matokeo ya msimu uliyopita kufutiliwa mbali na Shirikisho la Soka Kenya (FKF).

View Original Post on Mwanaspoti