Dewji: Motisha za Rais ni nzuri

Mwanaspoti
Published: May 25, 2023 17:10:01 EAT   |  Sports

MFADHILI wa zamani wa klabu ya Simba, Azim Dewji amesema motisha ambazo zinatolewa na Rais wa Jamhuri wa Muungano, Dk Samia Suluhu Hassan kwenye timu za Simba na Yanga zimechangia kwa kiasi kikubwa mafanikio ya timu hizo msimu huu. Dewji amesema kitendo cha Rais kutoa ahadi ya fedha kwa timu hizo kumechangia kwa timu kuongeza morali na kupambania timu pamoja na bendera ya nchi. "Rais wetu alianza kwa kutoa ahadi kwa kadri mechi zilivyokuwa zinaenda mbele ni kitu kikubwa na kizuri kwa sababu kimetoka kwake kwahiyo imeongeza morali; "Pesa ambayo anatoa ni kama sh 200 milioni kwa sababu ametoa Rais, hata sasa hii sh 20 milioni ni zaidi ya sh 200 milioni maana ni motisha kubwa kwa timu katika mchezo wa fainali,"amesema Dewji. Dewji amesema kwa upande wao licha ya kutoka kwenye hatua ya robo fainali ana imani kubwa viongozi wanatakiwa kujipanga katika msimu ujao kuhakikisha hawarudii makosa yaliyojitokeza msimu huu. "Unajua hizi Simba na Yanga zina mashabiki hawa 40 milioni kwahiyo naweza kusema nao ni serikali, haipendezi kuona Simba ikirudia makosa yale yale kwenye msimu ujao."