Watu 6 wanaodaiwa kumuua AKA wafikishwa mahakamani

Milard Ayo
Published: Feb 29, 2024 10:26:53 EAT   |  Entertainment

Siku moja baada ya Polisi wa South Africa kuthibitisha kuwa wamewamakata Washukiwa sita wa mauaji ya Rapper Kiernan Forbes maarufu AKA na kusema miongoni mwao ni ‘Mastermind’ aliyeandaa mpango mzima na kulipa Wauaji wote walioshiriki tukio hilo la February 10 2023, hatimaye leo Washukiwa watano wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Durban. Baba Mzazi wa AKA, […]

Siku moja baada ya Polisi wa South Africa kuthibitisha kuwa wamewamakata Washukiwa sita wa mauaji ya Rapper Kiernan Forbes maarufu AKA na kusema miongoni mwao ni ‘Mastermind’ aliyeandaa mpango mzima na kulipa Wauaji wote walioshiriki tukio hilo la February 10 2023, hatimaye leo Washukiwa watano wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Durban.

Baba Mzazi wa AKA, Tony Forbes ni miongoni mwa waliohudhuria Mahakamani hapo leo ambapo awali alifanya mahojiano akilalamikia kitendo cha Watuhumiwa hao kuruhusiwa kuficha sura zao lakini baadaye Mahakama ikawaamuru Washtakiwa kuonesha sura zao.

Mshtakiwa Mwenye umri mkubwa kati yao ni Mziwethemba Myeza mwenye umri wa miaka 36, wengine ni Lindani Ndimande (35), Siyanda Myeza (21), Lindokuhle Thabani (30) na Lindokuhle Ndimande (29).

Mshtakiwa wa kwanza kwenye kesi hiyo hiyo ni Muandaaji Mkuu ‘Mastermind’, pia wamo Watumia bunduki wawili, watoa taarifa wawili na mmoja wa mwisho ni aliyehusika kutafuta silaha na magari.

Waziri anayehusika na Idara ya Polisi Bheki Cele jana alisema miongoni mwa waliokamatwa wamewahi kuhusishwa na mauaji ya kutisha ambapo walikimbilia Nchi jirani ya Eswatini ( zamani Swaziland) kujificha lakini tayari wamekamatwa na taratibu za kuwarejesha South Africa zilishaanza kufanyiwa kazi