Simba SC imemteua Mels kuwa skauti wake Mkuu

Milard Ayo
Published: May 25, 2023 12:55:54 EAT   |  Sports

Simba Sports Club imemteua Mels Daalder kuwa skauti wake Mkuu. Mels ni raia wa Uholanzi mwenye uzoefu wa kufanya skauti kwenye timu mbalimbali. Mels ameshiriki kozi mbalimbali za scouting duniani ikiwa ni pamoja na kozi zikizoendeshwa na skauti wa zamani wa Manchester United, David Hobson. Mels ambaye ameshawahi kuishi Tanzania, ni shabiki mkubwa wa Simba […]

Simba Sports Club imemteua Mels Daalder kuwa skauti wake Mkuu. Mels ni raia wa Uholanzi mwenye uzoefu wa kufanya skauti kwenye timu mbalimbali.

Mels ameshiriki kozi mbalimbali za scouting duniani ikiwa ni pamoja na kozi zikizoendeshwa na skauti wa zamani wa Manchester United, David Hobson.

Mels ambaye ameshawahi kuishi Tanzania, ni shabiki mkubwa wa Simba pia ni mjuzi wa kufanya upembuzi (analysis) na ana ujuzi mkubwa na ufahamu mkubwa wa ligi ya Tanzania, Afrika Mashariki na
Afrika.

Mels anaongea lugha kadhaa ikiwemo; Kiholanzi, Kingereza, Kijerumani, Kifaransa na Kiswahili kwa kiasi fulani.

Akizungumza juu va uteuzi wa Mels; Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba Sports Club Imani Kajula amesema ” Tunafuraha kubwa kumkaribisha Mels ili kuja kuboresha ufanisi kwenye scouting kwani ni eneo muhimu sana kwenye mafanikio ya klabu yetu.

Tunaendelea na maboresho muhimu kuelekea msimu mpya wa ligi na mashindano ya kimataifa.