Sentensi za Mkurugenzi wa Wanachama Yanga SC ‘Tiketi 18,213 zimenunuliwa kuelekea mchezo dhidi ya USM Alger’

Milard Ayo
Published: May 25, 2023 12:52:07 EAT   |  Sports

Ni Young Africans ambapo leo Mei 25, 2023 imefanya Mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu kuelekea mechi ya Jumapili hii katika Uwanja wa Mkapa. Akizungumza na Waandishi wa habari katika Mkutano huo Mkuurugenzi wa Wanachama na Mashabiki Young Africans SC Haji Mfikirwa alisema..’Mpaka sasa wadau wameshanunua tiketi 18,213 na tunawaomba kuwasisitiza wadau ambao wametoa ahadi ya […]

Ni Young Africans ambapo leo Mei 25, 2023 imefanya Mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu kuelekea mechi ya Jumapili hii katika Uwanja wa Mkapa.

Akizungumza na Waandishi wa habari katika Mkutano huo Mkuurugenzi wa Wanachama na Mashabiki Young Africans SC Haji Mfikirwa alisema..’Mpaka sasa wadau wameshanunua tiketi 18,213 na tunawaomba kuwasisitiza wadau ambao wametoa ahadi ya manunuzi ya tiketi hizo kukamilisha ahadi yao kwa wakati pia Klabu itaandaa utararibu mzuri wa ugawaji wa tiketi hizi ili kuwafikia wengi, tutangalia pia watu kutoka mikoani tuone namna ambavyo tutawafikia pia” Mkurugenzi wa Wanachama na Mashabiki Young Africans SC Haji Mfikirwa.

“Tulianza kwenda kwenye vyuo mbalimbali lakini kwa sasa tumesitisha utaratibu huo, tutazingatia mambo kadha wa kadha kuelekea utaratibu mpya, kwanza tungependa kuwaomba wale ambao watapewa tiketi wafike uwanjani na yoyote atakayepewa tiketi tungeomba wasiuze tiketi hiyo kufanya hivyo ni kukiuka malengo na matarajio ya klabu” Mkurugenzi wa Wanachama na Mashabiki Young Africans SC Haji Mfikirwa