Milard Ayo   
RC Malima ataka kuifungua Ulanga

Published: May 25, 2023 17:02:29 EAT   |  News

Mkuu wa Mkoa Morogoro Adam Malima amesema endapo changamoto ya miundombinu ya Barabara na umeme katika Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga itapatiwa ufumbuzi wa kudumu itasadia milango na kuongeza wawekezaji ndani ya Halmashauri hiyo na kuanza kuongeza mapato RC Malima ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri hiyo ambapo amesema kukosekana kwa miundombinu madhubuti […]

Mkuu wa Mkoa Morogoro Adam Malima amesema endapo changamoto ya miundombinu ya Barabara na umeme katika Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga itapatiwa ufumbuzi wa kudumu itasadia milango na kuongeza wawekezaji ndani ya Halmashauri hiyo na kuanza kuongeza mapato

RC Malima ameyasema hayo wakati akizungumza na watumishi wa Halmashauri hiyo ambapo amesema kukosekana kwa miundombinu madhubuti ndani ya Halmashauri hiyo kunadhoofisha ukuaji wa kiuchumi.

Amesema suala la Barabara na Umeme ni muhimu kutokana na wilaya hiyo kuwepo na madini ya aina nyingi jambo ambalo wawekezaji wamekua wakiwasili kila siku hivyo uwepo wa miundombinu hiyo inaongeza hamasa kwa wageni kuja kuwekeza

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Dokta Julius Ningu amesema licha ya uwepo wa madini katika wilaya hiyo shughuli za kilimo na ufugaji nao umekua unachangia kwa kiasi kiubwa ukusanyaji wa mapato .

Ningu anasema kwa Mwaka wa fedha 2022/2023 wamejiwekea lengo la kukusanya mapato BIL.2.7 lakini hadi sasa wameshakusanya Bil. 2.1

Pamoja na hayo DC Ningu amesema changamoto kubwa ya wilaya hiyo ni Migogoro ya Wakulima na Wafugaji ambapo kwa sasa jitihada mbalimbali zinaendelea ili kutatua kero hiyo ikiwemo mikutano ya hadhara na kuongea na wafugaji na wakulima kuwaemisha umuhimu wa jamii hizo katika nchi.

 

.
.
.

 

View Original Post on Milard Ayo