Rais wa Afrika ya Kati kuitisha kura ya maoni kuhusu katiba mpya

Milard Ayo
Published: May 31, 2023 08:49:53 EAT   |  News

Rais Faustin Archange Touadera wa Jamhuri ya Afrika ya Kati alisema Jumanne kwamba ataitisha kura ya maoni kuhusu katiba mpya ambayo itamruhusu kuwania muhula mpya. “Nimeamua kuwasilisha mpango huu wa katiba mpya kwa kura ya maoni,” alisema katika hotuba kwa taifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa Facebook, bila kusema ni lini kura hiyo itafanyika. Wapinzani wa […]

Rais Faustin Archange Touadera wa Jamhuri ya Afrika ya Kati alisema Jumanne kwamba ataitisha kura ya maoni kuhusu katiba mpya ambayo itamruhusu kuwania muhula mpya.

“Nimeamua kuwasilisha mpango huu wa katiba mpya kwa kura ya maoni,” alisema katika hotuba kwa taifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa Facebook, bila kusema ni lini kura hiyo itafanyika.

Wapinzani wa Touadera tayari wamemshutumu kwa kutaka kurefusha utawala wake licha ya ukomo wa kikatiba.

Touadera alichaguliwa mnamo 2016 na alirudishwa kwa muhula wa pili mnamo 2020, licha ya shutuma nyingi za dosari za uchaguzi.

Mnamo Oktoba, alimuondoa jaji mkuu wa nchi hiyo, Daniele Darlan, katika kile wakosoaji walichokishutumu kama “mapinduzi ya kikatiba” baada ya kupinga amri za rais zilizolenga kurekebisha katiba.

Hivi sasa rais anaweza kuhudumu mihula miwili pekee.

“Hakutakuwa na muhula wa tatu, lakini hesabu itarejeshwa hadi sifuri, hivyo mtu yeyote anaweza kutafuta muhula mpya, ikiwa ni pamoja na Touadera kama anataka,” mshauri mkuu wa rais, Fidele Gouandjika, aliiambia AFP baada ya tangazo hilo.