PSG wachukizwa na Chelsea kukwamisha usajili wa Ziyech

Milard Ayo
Published: Feb 01, 2023 11:35:09 EAT   |  General

Club ya PSG ya Ufaransa imeelezwa kuwa imesikitishwa na kitendo cha club ya Chelsea kukosea kutuma nyaraka za usajili wa Hakim Ziyech mara mbili bila kuwa zimesainiwa kitu ambacho kimekwamisha usajili wa mkopo wa mchezaji huyo. Hakim alikuwa amekubaliana na club yake ya Chelsea kuwa aende kwa mkopo PSG na alikuwa tayari kawasili Paris kwa […]

Club ya PSG ya Ufaransa imeelezwa kuwa imesikitishwa na kitendo cha club ya Chelsea kukosea kutuma nyaraka za usajili wa Hakim Ziyech mara mbili bila kuwa zimesainiwa kitu ambacho kimekwamisha usajili wa mkopo wa mchezaji huyo.

Hakim alikuwa amekubaliana na club yake ya Chelsea kuwa aende kwa mkopo PSG na alikuwa tayari kawasili Paris kwa ajili ya kukamilisha usajili huo siku ya mwisho ya dirisha dogo lakini kukwama kwa usajili huo sasa ni wazi Ziyech atatakiwa kurejea London kuendelea kuitumikia Chelsea kwa miezi sita ijayo.

Kocha wa PSG Christophe Galtier

Kocha wa PSG Christophe Galtier alikuwa akitafuta winga na Ziyech alikuwa ni miongoni mwa machaguo yake katika maamuzi yake ya kwanza, Hakim alitaka kuondoka Kutokana na kupata nafasi ya kucheza game 10 katika Ligi Kuu England msimu huu.