Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii agusia suala la mgogoro uliopo katika Halmashauri ya Ushetu

Milard Ayo
Published: Feb 01, 2023 13:47:11 EAT   |  News

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja amewaomba Wananchi wa Jimbo la Ushetu kuwa watulivu wakati huu ambapo Serikali inapanga kushughulikia mgogoro uliopo katika Halmashauri ya Ushetu pamoja na Kaliuwa. Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni February 1, 2023 baada ya swali la nyongeza lililoulizwa na Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Emmanuel Cherehani […]

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja amewaomba Wananchi wa Jimbo la Ushetu kuwa watulivu wakati huu ambapo Serikali inapanga kushughulikia mgogoro uliopo katika Halmashauri ya Ushetu pamoja na Kaliuwa.

Kauli hiyo imetolewa leo Bungeni February 1, 2023 baada ya swali la nyongeza lililoulizwa na Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Emmanuel Cherehani aliyeomba kauli ya Serikali juu ya utatuzi wa mgogoro huo unaozidi kuchukua sura mpya ambapo mpaka kufikia hivi sasa Wananchi zaidi ya 17 wanashikiliwa na jeshi la Polisi.

“Niwaombe wananchi wa Ushetu wawe na subra, tulipanga kwenda kufanya mazungumzo na wananchi lakini ratiba zikaingiliana. Niwaombe wawe wavumilivu baada ya Bunge hili tutaondoka na Mbunge wao kwenda kuzungumza na kutatua changamoto hiyo”-