Mzee Mwinyi alivyowapa faraja wafiwa msiba wa Magufuli, ‘Wote walicheka hoi’- RIP Mwinyi

Milard Ayo
Published: Feb 29, 2024 20:44:52 EAT   |  News

Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Tanzania, Ally Hassan Mwinyi amefariki Dunia leo Februry 29,2024 saa 11:30 jioni Hospitalini Jijini Dar es salaam alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa saratani ya mapafu. Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza msiba huo leo ambapo amesema Mzee Mwinyi ambaye alikuwa Rais kuanzia mwaka 1985 hadi 1995, amekuwa akipatiwa […]

Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Tanzania, Ally Hassan Mwinyi amefariki Dunia leo Februry 29,2024 saa 11:30 jioni Hospitalini Jijini Dar es salaam alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa saratani ya mapafu.

Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza msiba huo leo ambapo amesema Mzee Mwinyi ambaye alikuwa Rais kuanzia mwaka 1985 hadi 1995, amekuwa akipatiwa matibabu tangu November 2023 London Uingereza na baadaye kurejea Nchini na kuendelea na matibabu Jijini Dar es salaam.

Rais Samia ametangaza siku saba za maombolezo kuanzia kesho kufuatia kifo hicho.

Hapa nimekusogezea Ufahamu enzi za uhai wake alichozungumza kwenye msiba wa Hayati John Pombe Magufuli.