Msanii wa South Africa aliewahi kushirikishwa na Diamond kwenye ‘Shu’, kuimba live Elements Masaki Feb 29

Milard Ayo
Published: Feb 29, 2024 16:08:43 EAT   |  Entertainment

Ni Mkali kutokea Afrika Kusini, Chley ambae rekodi zake aliwahi kuziandika Tanzania baada ya kusikika kwenye moja ya collabo aliyoshirikishwa na Diamond Platnumz kwenye hit single iitwayo Shu. Sasa Good news ninayotaka kukusogezea ni kwamba staa huyo Chley usiku wa leo Feb 29, 2024 anatarajiwa kutumbuiza na kuwaimbia Watanzania kwenye chimboi liitwalo Elements Masaki jijini […]

Ni Mkali kutokea Afrika Kusini, Chley ambae rekodi zake aliwahi kuziandika Tanzania baada ya kusikika kwenye moja ya collabo aliyoshirikishwa na Diamond Platnumz kwenye hit single iitwayo Shu.

Sasa Good news ninayotaka kukusogezea ni kwamba staa huyo Chley usiku wa leo Feb 29, 2024 anatarajiwa kutumbuiza na kuwaimbia Watanzania kwenye chimboi liitwalo Elements Masaki jijini Dar es Salaam.

Chley ni miongoni mwa wasanii wanaowakilisha vyema nchi yao hususani kupitia muziki wao unatamba kwasasa unaojulikana kwa jina la Amapiano.