Mkuu wa Wilaya ya Korogwe aandaa mbio za Mama wajawazito ‘MAMATHON’

Milard Ayo
Published: May 25, 2023 12:52:15 EAT   |  Educational

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Jokate Mwegelo ameandaa mbio za Mama wajawazito Wilayani Korogwe ambazo zimepewa njina la ‘MAMATHON’ lengo likiwa ni ni kutoa elimu na kuhamasisha wajawazito juu ya umuhimu wa kufatilia afya zao hususani kwenye suala la mazoezi na lishe bora kwa Mama na Mtoto. Akiongea na Waandishi wa Habari Wilayani Korogwe leo, […]

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Jokate Mwegelo ameandaa mbio za Mama wajawazito Wilayani Korogwe ambazo zimepewa njina la ‘MAMATHON’ lengo likiwa ni ni kutoa elimu na kuhamasisha wajawazito juu ya umuhimu wa kufatilia afya zao hususani kwenye suala la mazoezi na lishe bora kwa Mama na Mtoto.

Akiongea na Waandishi wa Habari Wilayani Korogwe leo, DC Jokate amesema mbio hizo ambazo hazina kiingilio (ni bure) zitafanyika Jumapili May 28,2023 ambapo pia kupitia mbio hizo watajikita katika kutoa elimu kwa vitendo pamoja na kugawa vifaa vya kujifungulia kwa Wajawazito.

“Dhamira ni kuwafikia wajawazito 2000 ambao wako tayari kujifunza kuhusiana na afya ya uzazi, ushauri juu ya lishe bora na mazoezi kipindi cha ujauzito na baada ya kujifungua”

“Siku ya mbio hizo tutakuwa na Matembezi ya kina Mama wajawazito, mafunzo kutoka kwa Wataalamu kuhusu umuhimu wa mazoezi na lishe bora kipindi cha ujauzito na baada ya kujifungua, tutatoa mafunzo pia juu ya mradi wa M-MAMA na jinsi ya kupata huduma hii na umuhimu wake”-Jokate Mwegelo 

“Washiriki watapata bure huduma ya kupima vipimo vya afya kama vile; presha, wingi wa damu, kipimo cha sukari na vipimo vingine muhimu vya afya, pia watapokea misaada ya vifaa tiba kwa ajili ya vituo vya afya na Hospitali yetu ya Wilaya, pamoja na ugawaji wa medali na tisheti kwa Washiriki wote”- Jokate Mwegelo 

.
.
.
.
.
.