‘Milango iko wazi kwa Wawekezaji wa Nishati Tanzania’- Waziri Makamba

Milard Ayo
Published: Feb 01, 2023 18:28:49 EAT   |  News

WIZARA YA NISHATI  yafungua rasmi Mkutano wa siku 3  wa Wadau wa Sekta ya Nishati nchini kutoka Mataifa mbalimbali  Jijini Dar es salaam Akizungumza na Wanahabari Leo Februari 01,2023 Waziri wa Nishati Januari Makamba wakati akifungua  Mkutano huo kwa wa wawekezaji wa Sekta ya Nishati kutoka mataifa mbalimbali  Jijini Dar es salaam  amesema Serikali ipo […]

WIZARA YA NISHATI  yafungua rasmi Mkutano wa siku 3  wa Wadau wa Sekta ya Nishati nchini kutoka Mataifa mbalimbali  Jijini Dar es salaam

Akizungumza na Wanahabari Leo Februari 01,2023 Waziri wa Nishati Januari Makamba wakati akifungua  Mkutano huo kwa wa wawekezaji wa Sekta ya Nishati kutoka mataifa mbalimbali  Jijini Dar es salaam  amesema Serikali ipo tayari kuweka nguvu kwenye sekta  binafsi kuhakikisha Sekta hiyo inatoa fursa mbalimbali.

Hata hivyo Makamba amewatoa hofu wawekezaji hao kuwa Taasisi ni nchi yenye Amani katika uwekezaji.

“Tumewakaribisha wawekezaji tupo tayari kuhakikisha uwekezaji wao unakuwa wenye tija zaidi hata hivyo serikali ipo tayari kuweka nguvu kwa sekta binafsi kwa maslahi mapana ya kupiga hatua za kimaendeleo nchini Tanzania’- Waziri Makamba

Pia ametoa wito kwa wadau wa sekta hiyo kushiriki Mkutano huo wa siku 03 ambao unatoa nafasi ya kujifunza vitu mbalimbali pamoja na kubadilishana uzoefu.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya jumuiya ya watoa huduma katika Sekta ya Nishati na gesi Abdulsamad Abdulrahim amesema wadau ada wa sekta ya Nishati wametayarisha mkutano huo kwa kuona Tanzania ni nchi yenye amani na ina Kiongozi imara na shupavu pamoja na kuvutiwa na fursa zilizopo nchini.

“Tuna gesi nyingi na wawekezaji wengi wanakuja na hata wawekezaji hawa waliojitokeza kwenye Mkutano huu leo wameelezwa kuwa nchi hii imejaa fursa nyingi na inahitaji kupiga hatua kimaendeleo kupitia sekta ya Nishati mbadala,gesi”- Waziri Makamba

Pia ameeleza kuwa waziri Kamba amewapa taarifa kuwa kuna miradi takribani 20 inatarajiwa kusainiwa siku za karibuni.

“Inawapa wawekezaji imani kuwa kasi ya Wizara hiyo inapiga hatua kwa vitendo zaidi pia wawekezaji wanatamani kuona pesa zinafanya kazi katika miradi mbalimbali ipasavyo.”- Waziri Makamba

“Kuna wawekezaji wameonyesha mfano hai kuwa nchi zingine zimepiga hatua hivyo wametaka kueka ubia na nchi ya Tanzania na kuona inapiga hatua kubwa katika sekta ya Nishati.

Hata hivyo ametoa rai kwa viongozi mbalimbali kumpa ushirikiano Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt.Samia Suluhu Hassan kwenye juhudi zake za kuhakikisha Tanzania ina Maendeleo na wawekezaji kuendelea kuwekeza nchini Tanzania ili kuongeza ajira nyingi kwa wazawa.

Mkutano umeandaliwa na EnergyNet kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati, EWURA, TPDS na Tanesco.

.
.
.
.
.
.

.
.

.