Meek Mill na Andrew Tate waanzisha mzozo mkubwa juu ya madai ya ngono ya Diddy

Milard Ayo
Published: Feb 29, 2024 10:10:35 EAT   |  Entertainment

Meek Mill ameingia kwenye skendo hiyo na Andrew Tate kufuatia maoni ya kuhusu rapper huyo kushutumiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Diddy katika kesi iliyowasilishwa hivi karibuni. Mapema wiki hii, Rodney “Lil Rod” Jones, mtayarishaji ambaye alifanya kazi kwenye Albamu ya Diddy ya The Love: Off the Grid, alimshtaki Diddy kwa unyanyasaji wa kijinsia […]

Meek Mill ameingia kwenye skendo hiyo na Andrew Tate kufuatia maoni ya kuhusu rapper huyo kushutumiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Diddy katika kesi iliyowasilishwa hivi karibuni.

Mapema wiki hii, Rodney “Lil Rod” Jones, mtayarishaji ambaye alifanya kazi kwenye Albamu ya Diddy ya The Love: Off the Grid, alimshtaki Diddy kwa unyanyasaji wa kijinsia na katika sehemu moja ya karatasi za kisheria zinazosambazwa mtandaoni, zinasomeka:

“Bw. Combs alimfahamisha Bw. Jones kwamba alikuwa amefanya ngono na rapa (REDACTED), mwimbaji wa R&B (REDACTED), na Stevie J.”

Ingawa majina hayo mawili yalifichwa,inasemekana kuwa kwenye maelezo ya chini yaliyoambatanishwa kwa kila moja inashukiwa kwamba kesi hiyo inawahusu Meek na Usher kutokana na maelezo husika kusema:

“Ni mwanamuziki na rapa wa Philadelphia ambaye alitoka kimapenzi na Nicki Minaj” na “Aliimba kwenye Superbowl na alikuwa na mkazi wa Vegas.

Baada ya kuanza kukanusha madai hayo, Meek ndipo alipomjia mtu ambaye alianza maswali kwenye jukwaa la X zamani Twitter kusema:

“Kwa hiyo P Diddy alikuwa akifanya mapenzi na Meek Mill na Usher?”

Meek alijibu:”Je, ulikuwa ukisafirisha wanawake? Tf wrong wit you Brody,” 

Kisha Tate akajibu:

“Niliuliza swali tu kwa sababu kila mtu anasema ilifanyika hivyo. Ni kweli au la?”

Meek aliacha kujibishana baada ya hapo, lakini aliendelea kuongea dhidi ya tetesi za kujihusisha na mapenzi na Diddy kuwa fake news.