Mbunge Kingu asimama bungeni atoa wito kwa Serikali ‘Kuwepo Chuo cha kisasa kitachotoa mafunzo Jeshini’

Milard Ayo
Published: May 25, 2023 12:25:15 EAT   |  News

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Innocent Bashungwa amewasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 . Sasa miongoni mwa wabunge waliosimama  na kuchangia Hoja ni Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Immanuel Kingu. “Dunia inabadilika ninaamini Jeshi letu limefanya ukombozi wa mataifa ya Kusini na kulinda mataifa […]

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Innocent Bashungwa amewasilisha Bungeni Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024 .

Sasa miongoni mwa wabunge waliosimama  na kuchangia Hoja ni Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Elibariki Immanuel Kingu.

“Dunia inabadilika ninaamini Jeshi letu limefanya ukombozi wa mataifa ya Kusini na kulinda mataifa mengi duniani  ninatoa wito kwa Wizara husika kuhakikisha kuimarisha vifaa vyetu vya kijeshi viwe vifaa vya kisasa tunahitaji kuwa na miundombinu ya kisasa ili kusudi tuwe na uhakika taifa letu kuwa Salama na Mungu awapiganie wazalendo wote wanaopigiana taifa letu- Mbunge wa Singida Magharibi Elibariki Immanuel Kingu

“Mheshimiwa Spika natoa wito kwa Jeshi letu lipewe fursa la kujenga Chuo Kikuu cha kisasa ambacho kitaweza kutoa mafunzo kwa Wanajeshi wetu kwa kujifunza teknolojia za kisasa kwani Dunia imeshabadilika’- Mbunge Singida Magharibi Elibariki Immanuel Kingu