Mbosso na Boss wa Samsung mkutano wa wadau

Milard Ayo
Published: Mar 17, 2022 07:25:13 EAT   |  Technology

Kampuni ya Kielektroniki ya Samsung Afrika Mashariki imekutana na wadau wake wa kibiashara katika hoteli ya Hayatt Jijini Dar es Salaam wakiwemo wafanyabiashara na wasambazaji wa bidhaa zake zote kutoka pande zote za nchi ya Tanzania. Mkutano huo umeandaliwa na Bw. Tae Sun Lee, Mkurugenzi Mkuu mpya wa Kampuni ya Kielektroniki ya Samsung Afrika Mashariki.

Kampuni ya Kielektroniki ya Samsung Afrika Mashariki imekutana na wadau wake wa kibiashara katika hoteli ya Hayatt Jijini Dar es Salaam wakiwemo wafanyabiashara na wasambazaji wa bidhaa zake zote kutoka pande zote za nchi ya Tanzania.
 Mkutano huo umeandaliwa na Bw. Tae Sun Lee, Mkurugenzi Mkuu mpya wa Kampuni ya Kielektroniki ya Samsung Afrika Mashariki.

Lengo kuu la mkutano huo ni kuwaleta pamoja wadau wakuu wa bidhaa za Samsung wakiwemo wasambazaji na wafanyabishara ili kuhakikisha matumizi bora zaidi yanatolewa kwa mtumiaji wa bidhaa za Samsung.
Kampuni ya Samsung inaendelea kuamini kuwa maendeleo ya kiteknolojia ndio kichocheo kikuu cha biashara ya bidhaa zake ulimwenguni.

Katika mkutano huo, bidhaa mbalimbali za Kampuni ya Samsung za mwaka 2022 zimeonyeshwa zikiwemo simu ambapo bidhaa hizo zikilenga kikazi cha millennia, Z.
Akiongea wakati akiwasilisha mada katika Mkutano huo Mkurugenzi Mkuu wa Samsung Bw. Lee amesema kuwa Kampuni ya Samsung itaendelea kuimalisha mahusiano yao na washirika wao wakiwemo wasambazaji wote kutoka pande zote za Tanzania na ukanda mzima wa Afrika Mashariki.

Msanii wa muziki Mbosso akiwa na Mabosi wa Samsung Afrika katika mkutano wa wadau wa mawasiliano na wafanyabiashara .

Bwana Lee amesema kuwa Kampuni ya Samsung itaendelea kuhakikisha bidhaa zote zinazotengenezwa na Kampuni hiyo zinaendelea kuwa zenye ubora wa hali ya juu ili kumpa furaha na faraja mtumiaji wake.

Ameongezea kuwa mkakati mkubwa wa Kampuni ya Samsung ni kuendelea kuona bidhaa zake za kielektroniki zinaendelea kuwa bidhaa pendwa kabisa katika soko la Afrika.

Katika mkutano huo, Millicom Tanzania PLC [Tigo] wameweza kuanzisha mashirikiano na Kampuni ya Kieleckroniki ya Samsung ikiwa ni mpango kabambe wa kumuwezesha mteja anayetumia Samsung ‘Smart TV’ kuweza kupata kifaa cha kumuwezesha kutumia intanet kwenye luninga yake cha Mi-Fi kutoka Tigo.

Katika makubaliano hayo, mteja atakaye atanunua luninga ya Samsung smart katika kipindi cha ofa ataweza kupata kifaa hicho cha MiFi kutoka Kampuni yaTigo kikiwa na kifurushi cha kuanzia ili kumuwezesha kujiunga na mtandao wa intanet katika luninga yake

Naye, Afisa Mkuu (Mikakati na Ubunifu) wa Kampuni ya Tigo David Umoh amesema: “Kama Tigo, kupitia teknolojia tunalenga kufanya maisha ya Mtanzania kuwa bora zaidi ndiyo maana tumeamua kushirikiana na Kampuni ya Samsung katika kuhakikisha kila mteja atakaye nunua Smart TV ya Samsung anapata kifaa cha intanet cha MiFi kutoka Tigo.”

Bwana Umoh ameongezea kuwa kampuni ya Samsung imekuwa mmoja wa washirika wao wakuu nchini Tanzania na amesisitiza kuwa wataendelea kufanya kazi pamoja ikiwa ni katika mipango chanya ya kuhakikisha maisha ya Mtanzania yanakuwa bora zaidi.

Zaidi ya hayo, Kampuni ya kielectroniki ya Samsung iliunganisha pamoja kitengo chake cha simu pamoja na kile cha watumiaji wa bidhaa mbali mbali kuwa kitengo kimoja cha DX.

Lengo kuu la kuweza kuwa na kitengo kimoja ni kumuwezesha mtumiaji wa bidhaa za Samsung kupata huduma zote sehemu moja.

Kampuni ya Samsung imetanabahisha kuwa wataendelea kutengeneza bidhaa mbalimbali na kutoa huduma bora zaidi ili kuendela kudumisha mahusiano yao na watumiaji.

“Kama Samsung tunasisitiza kuwa tutaendelea kuwa na sauti moja pale tunapoweka mikakati yetu ili tuweze kwenda mbele. Mienendo yetu ya soko inaendelea kubadilika na pia tunaona haja ya kurekebisha katika maeneo mbali mbali ili kukidhi mahitaji ya wadau,” Bw. Tae Sun Lee, Mkurugenzi Mkuu, Samsung Electronics Afrika Mashariki alisema.

Mkutano huo ulioandaliwa na Kampuni ya Samsung ulihudhuriwa na wadau mbali mbali wa Kampuni hiyo wakiwemo wafanyabiashara zaidi ya 100 waliokutana na kujadili mahitaji ya soko na jinsi gani kwa pamoja wanaweza kukuza soko la Samsung nchini Tanzania.