Madiwani Ngorongoro waigomea Rasimu ya mpango wa matumizi ya ardhi “Madiwani hawajui kiingereza”

Milard Ayo
Published: May 25, 2023 15:08:07 EAT   |  Travel

Madiwani wa Baraza la Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro Mkoa wa Arusha,wameikataa rasimu ya mpango wa matumizi ya Ardhi ya wilaya hiyo, wakidai si shirikishi na inalenga kumega ardhi yao ya malisho na kuiingiza kwenye hifadhi kitendo ambacho wamedai kitaathiri ustawi wa Wananchi . Madiwani hao walitoa kauli hiyo katika baraza hilo la madiwani baada […]

Madiwani wa Baraza la Halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro Mkoa wa Arusha,wameikataa rasimu ya mpango wa matumizi ya Ardhi ya wilaya hiyo, wakidai si shirikishi na inalenga kumega ardhi yao ya malisho na kuiingiza kwenye hifadhi kitendo ambacho wamedai kitaathiri ustawi wa Wananchi .

Madiwani hao walitoa kauli hiyo katika baraza hilo la madiwani baada ya kuwasilishwa kwa ajenda namba nne katika kikao hicho iliyolenga kujadili na kupitisha mpango wa matumizi ya Ardhi wa miaka 20 kuanzia mwaka huu 2023 hadi 2043.

Diwani wa kata ya Nainokanoka,Edward Maura alisema hawakubaliani na rasimu hiyo kwa kuwa imelenga kuchukua sehemu kubwa ya Ardhi yao na kuifanya sehemu ya eneo la hifadhi jambo litakaloathiri ustawi wa maisha yao na malisho ya mifugo.

Maura ambaye pia ni mwenyekiti wa baraza la wafugaji alifafanua kuwa ,wilaya ya Ngorongoro inakata 28,vijiji 72 ikiwa na ukubwa wa Ardhi ya kilometa za mraba 14,030 na asilimia 75 ni hifadhi na asilimia 25 ni matumizi ya wananchi ikiwemo malisho ,hivyo kupitisha rasimu hiyo ni kuhatarisha makazi ya wananchi wapatao 274,000.

“Sisi kama madiwani tumeweka saini zetu kwa pamoja kukataa rasimu hiyo na sababu za kukataa ni pamoja na serikali kuchukua eneo letu kubwa na kubakiwa na asilimia 25 tu”alisema

Aliongeza kuwa mpango wa matumizi ya Ardhi wa wilaya ya Ngorongoro haukufuata matakwa ya sheria ya kushirikisha mikutano mikuu halali ya vijiji ,hivyo kupitisha mpango huo ni kuhalalisha mwisho wa kuishi kwa kuendelea kukosa makazi,kilimo na nyanda za malisho.

Naye diwani wa viti maalumu kata ya Kakesio, tarafa ya Ngorongoro ,Sein Lekeni alisema sababu ya kukataa rasimu hiyo ni kutoshirikishwa kwa wananchi na kupewa elimu juu ya umuhimu wa jambo hilo na iwapo tutaikubali tutakuwa watu wa ajabu sana .

 

“Leo tulikuwa kwenye kikao cha baraza la madiwani , tumekataa ile rasimu iliyokuwa imeletwa kwenye baraza kwa sababu sio shirikishi ni rasimu ambayo imepangwa na watu fulani ,na tukipitisha tutakuwa madiwani wa ajabu sana ,sisi sote madiwani 32 tumeikataa kwa kuweka saini zetu ”

Diwani mwingine ,James Moringe wa kata ya Laitore,alisema ajenda ya matumizi ya ardhi ya miaka 20 katika wilaya ya Ngorongoro haina tija na wameikataa kwa sababu imetenga wilaya hiyo kijiografia .

 

Alisema utaratibu kama huo uliwahi kutumiwa na serikali kupima eneo lao la malisho lenye ukubwa wa kilometa za mraba 1500 na kulifanya pori tengefu kinyume cha sheria ,suala waliosisitiza kuwa hawakubaliani na rasimu hiyo.

“Hakuna mikutano ya wananchi iliyotumika kuzungumzia suala hilo kuanzia tarafa ya Ngorongoro ambako ndio yaliko makazi ya wamasai”

Kwa upande wake Mwenyekiti wa baraza hilo la Madiwani,Mohamed Bayo alisema kuwa raimu hiyo haikuweza kupita kwa sababu iliandikwa kwa Lugha ya Kiingereza na madiwani wa jamii ya wafugaji wengi wao hawajui kiingereza hivyo niliamuru ikafanyiwe marekebisho.

Hata hivyo mwenyekiti huyo alisema anakubaliana na ras
imu hiyo ila alisema lazima ifanyiwe marekebisho kwani hakuna serikali inayochukia wananchi wake na anaimani mpango wa serikali ni mzuri .