Lil Wayne ajinadi kuwa rapa bora wa Hip Hop “G.O.A.T”

Milard Ayo
Published: Feb 27, 2023 12:00:14 EAT   |  Entertainment

Legendaries wa Hip-hop wamekuwa wakijadili kwa wiki kadhaa kuhusu orodha mpya ya rapa bora zaidi wa muda wote ambayo Jay-Z anashika nafasi ya 1 lakini chakushangaza ni kwamba sasa Lil Wayne ameingia kwenye gumzo na anasema yeye ndiye G.O.A.T. Yaani “Greatest Of All Times” Weezy alisema hayo wiki iliyopita wakati alipokuwa kwenye podcast ya Muziki […]

Legendaries wa Hip-hop wamekuwa wakijadili kwa wiki kadhaa kuhusu orodha mpya ya rapa bora zaidi wa muda wote ambayo Jay-Z anashika nafasi ya 1 lakini chakushangaza ni kwamba sasa Lil Wayne ameingia kwenye gumzo na anasema yeye ndiye G.O.A.T. Yaani “Greatest Of All Times”

Weezy alisema hayo wiki iliyopita wakati alipokuwa kwenye podcast ya Muziki ya Apple ya Zane Lowe, ambapo mada ya Rapa 50 bora kwenye billboard wa muda Wote ambayo iliyochapishwa Februari 8 ilipotoka na kwa mshangao wayne aliingia kwenye #7 tu, chini ya zingine kadhaa.

Kwenye list yupo Biggie, Eminem, Tupac, Nas, Kendrick Lamar na Jay-Z mbele yake, lakini Wayne aliomba kutofautiana na hao wote, hasa miongoni mwa wale ambao bado wapo kwenye game na moja kwa moja, yeye ni namba 1 na ni mkuu kuliko wao.

Ukifuatilia upande wa mtandao wa  Twitter inaonekana wengi wanakubaliana na dhana kwamba Wayne, kwa kweli, ni bora kuliko Jay-Z katika masuala ya uwezo wa kurap na ukweli ni kwamba, Weezy bado yuko kwenye chart ya mwaka wa 2023 tofauti na jay-z alipo sasa.

Mpaka sasa idadi yao ya hits songs inalingana Wayne ana hits 3 #1 (Billboard Hot 100) na Jay-z ana 4 #1 zake mwenyewe lakini Wayne ana nyimbo 25 kati ya 10 bora kihistoria, wakati Jay ana nyimbo 22 tu