Guardiola anyakua tuzo ya tatu ya Meneja Bora wa Mwaka wa LMA!

Milard Ayo
Published: May 31, 2023 08:18:15 EAT   |  Sports

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amechaguliwa kuwa kocha bora wa mwaka na Chama cha makocha wa Ligi. Hii ni mara ya tatu kwa Guardiola kutwaa Tuzo hiyo inayoitwa ‘Sir Alex Ferguson Award’, iinayopigiwa kura na mameneja ama makocha wa madaraja yote ya ligi nchini England. Mhispania huyo, 52, pia alishinda tuzo ya kocha ama […]

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amechaguliwa kuwa kocha bora wa mwaka na Chama cha makocha wa Ligi. Hii ni mara ya tatu kwa Guardiola kutwaa Tuzo hiyo inayoitwa ‘Sir Alex Ferguson Award’, iinayopigiwa kura na mameneja ama makocha wa madaraja yote ya ligi nchini England.

Mhispania huyo, 52, pia alishinda tuzo ya kocha ama meneja bora wa mwaka wa ligi kuu England baada ya timu yake kunyakua taji la tatu mfululizo na la tano katika misimu sita. Kocha wa Chelsea, Emma Hayes alishinda kwa upande wa Ligi ya Wanawake ya Super League. Ilikuwa tuzo yake ya nne mfululizo na ya sita kwa jumla.

Guardiola amekuwa meneja wa tatu kushinda tuzo tatu au zaidi za kocha bora wa mwaka wa LMA, sawa na David Moyes, lakini bado yuko ya kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson mwenye tuzo 5.

Akizungumza baada ya kutwaa taji la LMA, Guardiola alisema: ‘Nimefurahi kupokea Meneja Bora wa Mwaka wa Ligi Kuu ya Uingereza. Ni heshima kubwa kupokea kombe lake.

‘Tuko kwenye ligi bora zaidi duniani na ninakuahidi tutakuwepo msimu ujao.’