GSM Group of Companies yatoa salamu za pole kufuatia msiba wa Rais Mstaafu Mwinyi

Milard Ayo
Published: Feb 29, 2024 22:50:47 EAT   |  News

Ni February 29, 2024 ambapo Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Tanzania, Ally Hassan Mwinyi amefariki Dunia saa 11:30 jioni Hospitalini Jijini Dar es salaam alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa saratani ya mapafu. Ikiwa ni saa chache baada ya kuenea na taarifa hiyo ya huzuni hapa tunao kampuni ya GSM ambao nao wameungana […]

Ni February 29, 2024 ambapo Rais Mstaafu wa awamu ya pili wa Tanzania, Ally Hassan Mwinyi amefariki Dunia saa 11:30 jioni Hospitalini Jijini Dar es salaam alipokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa saratani ya mapafu.

Ikiwa ni saa chache baada ya kuenea na taarifa hiyo ya huzuni hapa tunao kampuni ya GSM ambao nao wameungana na Watanzania wote katika kipindi hiki cha kuomboleza.

‘Uongozi wa Makampuni ya GSM GROUP tunatoa salamu za pole kwa watanzania na familia ya Rais mstaafu wa awamu ya pili Mhe.Ali Hassan Mwinyi aliefariki siku ya tarehe 29 February, 2024 jijini Dar es Salaam’- GSM Group of Companies

‘Tunaungana na Watanzania, ndugu, jamaa na Familia ya Marehemu kuomboleza msiba huu mkubwa, Sisi ni wa mwenyezi Mungu na kwake tutarejea, Mungu ampe kauli thabit’ – GSM Group of Companies