Milard Ayo   
Fei toto hajakubali yaishe, aomba mchango kwa Watanzania, kufungua kesi ‘CAS’

Published: May 25, 2023 16:00:11 EAT   |  Sports

Mchezaji Feisal Salum “Fei Toto” baada ya kugonga mwamba mara mbili TFF kwa kushindwa kukubaliwa ombi lake la kuvunja mkataba, Feisal ametangaza kuomba kuchangiwa pesa za kwenda Mahakama ya usuluhishi wa kimichezo (CAS) “Ndugu zangu Watanzania na familia yote ya soka kwa Bara na visiwani. Mimi kijana wenu ambaye kwa miaka yote nimekua na nidhamu […]

Mchezaji Feisal Salum “Fei Toto” baada ya kugonga mwamba mara mbili TFF kwa kushindwa kukubaliwa ombi lake la kuvunja mkataba, Feisal ametangaza kuomba kuchangiwa pesa za kwenda Mahakama ya usuluhishi wa kimichezo (CAS)

“Ndugu zangu Watanzania na familia yote ya soka kwa Bara na visiwani. Mimi kijana wenu ambaye kwa miaka yote nimekua na nidhamu nje na ndani ya uwanja na kwa dhati nimeitumikia klabu ya Yanga na Timu ya Taifa ya Tanzania na Zanzibar Heroes”

“Utiifu wangu umekua shubiri ya maisha yangu ya soka, nimevumilia nimeshindwa, sitamani tena mama yangu kutukanwa. TFF imeshindwa kunisaidia kupata haki yangu ya Kuvunja mkataba na Yanga hivyo nimeamua Kwenda Mahakama ya michezo CAS”

View Original Post on Milard Ayo