Amfungia mpenzi wake ndani kwa siku 3 kisa wivu wa mapenzi

Milard Ayo
Published: May 25, 2023 11:08:41 EAT   |  News

Mwanamke aliyetajwa kuwa mwenye wivu kupita kiasi nchini Argentina alikamatwa hivi majuzi kwa kumweka mpenzi wake kama mfungwa katika nyumba yake kwa siku tatu ili kuhakikisha kuwa hamlaghai. Jeshi la polisi katika jiji la Argentina la La Plata walimuokoa mwanamume mwenye umri wa miaka 29 kutoka kwenye chumba kilichokuwa kimefungwa kwenye nyumba ya mpenzi wake […]

Mwanamke aliyetajwa kuwa mwenye wivu kupita kiasi nchini Argentina alikamatwa hivi majuzi kwa kumweka mpenzi wake kama mfungwa katika nyumba yake kwa siku tatu ili kuhakikisha kuwa hamlaghai.

Jeshi la polisi katika jiji la Argentina la La Plata walimuokoa mwanamume mwenye umri wa miaka 29 kutoka kwenye chumba kilichokuwa kimefungwa kwenye nyumba ya mpenzi wake na alidai kuwa alifungiwa ndani kwa zaidi ya saa 72 kufuatia ugomvi na mpenzi wake wa miezi sita, ambaye alitokea kuwa na wivu kupita kiasi.

Baada ya kupata ujumbe kwenye ukurasa wa WhatsApp kutoka kwenye simu yake aliichukua na kuipasua  ili kumzuia asizungumze na wanawake wengine ndipo aliamua kumuweka ndani kwa siku tatu mfululizo, hadi alipoweza kwa namna fulani kuiba simu ya mwanamke wake  na kumtumia rafiki yake ujumbe kwaajili ya  msaada.

Wapenzi  hao wa zamani walikuwa wamechumbiana kwa miezi sita, lakini mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 30 alizidi kumwonea wivu mwanaume wake mwenye umri wa miaka 29, kila wakati.