Milard Ayo   
Ali Kamwe afunguka kuhusu shangwe ya Fainali ya CAF kuelekea mchezo dhidi ya USM Alger

Published: May 25, 2023 13:04:22 EAT   |  Sports

Ni Young Africans ambapo leo Mei 25, 2023 imefanya Mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu kuelekea mechi ya Jumapili hii katika Uwanja wa Mkapa dhidi ya USM Alger. “Jumamosi tutakuwa na Jogging la Fainali, Viongozi wote wa Yanga Sc wakiongozwa na Rais na Makamu wa Rais, pia Wasafi Jogging na vikundi vingine vya Jogging vinakaribishwa. […]

Ni Young Africans ambapo leo Mei 25, 2023 imefanya Mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu kuelekea mechi ya Jumapili hii katika Uwanja wa Mkapa dhidi ya USM Alger.

“Jumamosi tutakuwa na Jogging la Fainali, Viongozi wote wa Yanga Sc wakiongozwa na Rais na Makamu wa Rais, pia Wasafi Jogging na vikundi vingine vya Jogging vinakaribishwa. Njoo tuweke mwili sawa kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Fainali”- Afisa Habari wa Young Africans SC

Siku ya ijumaa tutakuwa na Shangwe ya FAINALI ya CAF, Shangwe hili tutaifanyia pale MBAGALA ZAKHEM itaanza saa 6 mchana, kwenye SHANGWE hili makundi yetu ya hamasa ya Yanga yatapaswa kufika eneo hilo, wadau wetu na watu mashughuli tunawaasa sana wafike eneo hilo hapatatosha hayo ndio maandalizi ya kwenda KUMKANDA mwarabu”- Afisa Habari wa Young Africans SC

Tiketi za mchezo wetu wa fainali #cafcc Jumapili zinapatikana katika maduka ya TTCL nchi nzima na vituo tajwa.

.

View Original Post on Milard Ayo