From: 2023-10-06 to: 2023-10-19
( )
MHASIBU - 1 POST
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Duties & Responsibilities

Kushiriki katika utayarishaji wa bajeti ya Programu na kufanya ufuatiliaji na kusimamia mapato na matumizi ya fedha za Programu kwa kuzingatia Mpango na bajeti iliyoidhinishwa;

ii.Kutayarisha taarifa za kifedha na kibenki za kila mwezi, robo mwaka na mwaka za utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Programu, na kuziwasilisha kwenye Timu ya Usimamizi wa Programu;

iii.Kufuatiia kwa ukaribu matumizi ya fedha za Programu na kuhakikisha kuwa matumizi hayo yanazingatia Sheria, Kanuni na Taratibu zinazosimamia matumizi ya fedha za umma, miongozo ya Programu na Mpango na bajeti iliyoidhinishwa kwa mwaka wa fedha husika;

iv.Kutayarisha taarifa za hali ya kifedha (financial statements) za programu na kuziandaa kwa ajili ya ukaguzi wa ndani na nje ya taasisi kwa kuzingatia Miongozo ya Serikali na Programu;

v.Kuchambua taarifa za kifedha za Programu kwa lengo la kubaini changamoto za utekelezaji na kuishauri Timu ya Usimamizi wa Programu namna ya kutatua changamoto hizo;

vi.Kutoa ushauri kwenye Timu ya Usimamizi wa Programu kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu udhibiti na usimamizi wa fedha za Programu ili kuongeza ufanisi wa usimamizi wa fedha hizo; na 

vii.Kufanya kazi nyingine zozote za fani yake atakazoagizwa na kupangiwa na Mkuu wake.

 

Qualifications

Awe na Shahada ya Kwanza ya Uhasibu, CPA na uzoefu kazini wa angalau Miaka 3. Shahada ya Uzamili ya Uhasibu itakuwa sifa ya ziada.

 

Remuneration

Kulingana na viwango vya Mradi