i.Kufanya kazi kwa vitendo katika fani usanifu majengo ili kumwezesha kupata sifa za kutosha kusajiliwa na Bodi ya Usajili inayowahusu Wasanifu majengo,
ii.Kufuatilia upatikanaji wa taarifa na taaluma za usanifu wa majengo,
iii.Kupitia mapendekezo ya miradi (project proposals) mbalimbali ya majengo yanayowasilishwa Wizarani.
Kuajiriwa wenye mojawapo ya sifa zilizotajwa hapa chini:
i.Waliohitimu kidato cha iv na kufuzu kozi ya ufundi ya miaka mitatu kutoka vyuo vya ufundi vinavyotambuliwa na Serikali katika mojawapo ya fani ya usanifu majengo
ii.Waliohitimu kidato cha vi na kufuzu mafunzo ya ufundi wa miaka miwili kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali katika mojawapo ya fani za usanifu majengo
iii.Wenye cheti cha majaribio ya Ufundi Hatua ya I katika mojawapo ya fani za usanifu majengo kutoka chuo cha ufundi kinachotambuliwa na Serikali,
iv.Wenye Stashahada ya kawaida katika katika mojawapo ya fani za usanifu majengo kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
FUNDI SANIFU - MAJENGO