From: 2023-10-06 to: 2023-10-19
( )
DAKTARI - 1 POST
Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
Duties & Responsibilities

i.Kushiriki katika kusaidia utayarishaji na utekelezaji wa Mikakati, Malengo, na Mipango ya Programu kwa kushirikiana na Timu ya Menejimenti ya Programu; 

 

ii.Kuratibu lojistiki na ratiba za vikao na matukio mbalimbali ya Programu ikijumuisha masuala ya ukumbi, usafiri na utunzaji wa muda, kwa kushirikiana na Msimamizi wa Programu (Program Administrator) na Afisa Ununuzi wa Programu; 

 

iii.Kusaidia katika kuimarisha mawasiliano na timu ya Usimamizi wa Programu, ikiwa ni

pamoja na kusikiliza changamoto za kila siku za utekelezaji wa Programu na kuzitafutia ufumbuzi; 

 

iv.Kusaidia katika kukusanya, kuchakata, kuchambua na kutunza takwimu ili kuwezesha 

kuanza kwa utekelezaji wa mchakato wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Programu; 

 

v.Kusaidia uratibu wa Rasilimali Watu, Magari, Vifaa na nyenzo nyingine za Programu, 

katika utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za Programu; 

 

vi.Kusaidia katika kukusanya taarifa mbalimbali za maendeleo ya utekelezaji wa Programu kwenye Sekretarieti za Mikoa, Halmashauri na Vituo vya kutolea huduma za afya, na kuziwasilisha kwenye timu ya Usimamizi wa Programu, kwa ajili ya matumizi ya ndani na nje ya Taasisi; 

 

vii.Kusimamia utekelezaji wa shughuli na afua mbalimbali za programu ili kuhakikisha

zinatekelezwa kwa ubora na viwango kama vilivyoainishwa kwenye Miongozo ya Programu;

 

viii.Kufanya uhamasishaji wa Programu kwenye ngazi ya Jamii na wanufaika wengine wa 

Programu, ili kuweza kupata mrejesho, maoni na kuungwa mkono katika utekelezaji wa Programu;

 

ix.Kufanya utafiti na kukusanya taarifa zinazohusiana na utekelezaji wa vipaumbele vya 

Programu, na kutoa machapisho kwa maeneo yaliyofanya vizuri na kushauri uboreshaji wa maeneo yenye changamoto kwa kuzingatia utaratibu wa utoaji wa mchapisho wa Taasisi; na

 

x.Kufanya kazi nyingine zozote za fani yake atakazoagizwa na kupangiwa na Mkuu wake.

1.5NGAZI YA MSHAHARA: Kulingana na viwango vya Mradi.

 

2.0KATIBU WA AFYA- NAFASI 1

2.1 SIFA ZA MWOMBAJI

Mwombaji awe na Shahada ya Uongozi wa Huduma za Afya (Health Services Administration) kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali pamoja na Shahada ya Uzamili ya katika moja ya fani ya Mfumo wa Taarifa za Uendeshaji wa Huduma za Afya (Health System Management) au Ufuatiliaji na Tathmini katika Sekta ya Afya (Health Monitoring and Evaluation) na awe na uzoefu kazini wa angalau miaka mitatu.  Mwombaji aliyefanya kazi kwenye Miradi/Programu, itakuwa sifa ya ziada.

 

2.2 KURIPOTI KWA: MRATIBU WA PROGRAMU

2.3 JUKUMU KUU

Katibu wa Afya ndiye Msimamizi wa Programu (Program Administrator), katika kupanga, kuratibu, kutekeleza, kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Programu kwa kushirikiana na Timu ya Usmiamizi wa Programu.

 

2.4 MAJUKUMU MAHSUSI

i.Kushiriki katika maandalizi ya Mipngo na Bajeti ya Programu ili kuhaikisha Malengo yaliyokusudiwa yanafikiwa;

ii.Kusimamia utengaji wa bajeti kwa fedha za Programu kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli na afua mbalimbali za Programu na kusimamia utekelezaji wa afua hizo;

iii.Kusimamia Rasilimali watu, Magari na Vifaa vya Programu, kwa kushirikiana na Timu ya Usimamizi wa Programu, ili kuhakikisha mafanikio yaliyokusudiwa yanafikiwa;

iv.Kushiriki katika ufuatiliaji na tathmini wa Programu ili kupima ufanisi na maendeleo ya utekelezaji wa shughuli na afua mbalimbali za Programu, kubaini changamoto na kuzipatia ufumbuzi ili programu iendelee kutekelezwa kwa ufanisi uliokusudiwa; 

v.Kushirikiana na Timu ya Usimamizi wa Programu, kuhakikisha Programu inatekelezwa kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Serikali, Taasisi na Miongozo inayosimamia utekelezaji wa Programu husuika;

vi.Kufuatiia na kusimamia ukusanyaji, uchakataji na uchambuzi wa taarifa za utekekezaji wa shughuli za Programu za mwezi, robo Mwaka na Mwaka na kuziwasilisha kwenye Timu ya Usimamizi wa Programu;

vii.Kuimarisha mawasiliano kati ya Taasisi na Wadau mbalimbali wa Programu, ikijumusha watumishi, Wahisani na Wadau wengine wa Programu;

viii.Kuhakikisha kuwa taarifa mbalimbali za Programu zinarekodiwa na kutunzwa vizuri na kwa usahihi, ikiwa ni pamoja na kuratibu utoaji wa machapisho ya programu; 

ix.Kuratibu shughuli za ufuatiliji zitakazofanywa na Mdau Benki ya Dunia (World Bank Mission activities), na kuhakikisha kuwa makubaliano yaliyofikiwa kati ya Serikali na Mdau wakati wa ufuatiliaji huo yanafanyiwa kazi kwa wakati; na

x.Kufanya kazi nyingine zozote za fani yake atakazoagizwa na kupangiwa na Mkuu wake.

Qualifications

Mwombaji awe na Shahada ya Udaktari wa Binadamu kutoka Vyuo Vikuu/Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali. Mwombaji awe amemaliza mafunzo ya Daktari wa Tiba (Doctor of Medicine- MD), mafunzo ya kazi “Internship” ya muda usiopungua mwaka mmoja na kupata usajili kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika), pamoja na Shahada ya Uzamili (Masters) ya Afya ya Sayansi ya Jamii (MPH) na awe na uzoefu kazini usiopungua wa miaka 3.  Uzoefu kwenye uratibu wa miradi itakuwa ni sifa ya ziada.

Remuneration

Kulingana na viwango vya Mradi