Taifa Leo General
Rais Ruto awasili akiwa amechelewa Embu kuadhimisha Madaraka Dei 2023    

  NA SAMMY WAWERU RAIS William Ruto alichelewa kuwasili katika Uwanja wa Moi, Embu ambako maadhimisho ya Madaraka Dei 2023 yanafanyika, Alhamisi, Juni 1. Dkt Ruto anaongoza taifa kuadhimisha Sikukuu hii ya Juni 1 kila mwaka, inayoandaliwa kusherekea Kenya kupata uhuru wa ndani kwa ndani kujitawala kutoka kwa serikali ya Mbeberu 1963. Kinyume na itifaki

1 day ago


Milard Ayo General
Real Madrid ndio klabu yenye thamani kubwa zaidi duniani kwa mujibu wa Forbes

Kwa mwaka wa pili mfululizo, Real Madrid ndiyo klabu yenye thamani kubwa zaidi ya kandanda duniani ikiwa na thamani ya dola bilioni 6.070, kulingana na Forbes. Chapisho la klabu hiyo linasema katika ripoti yake kwamba klabu yake imepata ongezeko la 19% la thamani ikilinganishwa na mwaka jana. Pia inaangazia mapato yanayotokana na Real Madrid kutokana

1 day ago


Milard Ayo General
NATO inajadili ‘dhamana ya usalama’ kwa Ukraine

Uvamizi wa Urusi nchini Ukraine mwezi Februari mwaka jana umeupa nguvu muungano wa kijeshi wa nchi za Magharibi ulioanzishwa takriban miaka 75 iliyopita kukabiliana na Umoja wa Kisovieti lakini kwa zaidi ya wiki tano tu kabla ya mkutano wa kilele wa viongozi wa NATO katika mji mkuu wa Lithuania Vilnius kuna migawanyiko katika masuala muhimu.

1 day ago


Mwanaspoti Sports
Phiri uhakika Simba, wakaa na kocha

Zilikuwepo taarifa za straika wa Simba, Moses Phiri kutaka kusepa kutokana na kushindwa kupata nafasi kikosi cha kwanza baada ya kutoka kuuguza majeraha, upepo umebadilika staa huyo ataendelea kusalia Msimbazi. Ipo hivi; Imeelezwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba, Salum Abdallah 'Try Again' alimwita Phiri na kumkalisha chini, ili kumweleza bado wanamhitaji kwenye kikosi, hivyo wakakubaliana kwa amani na sasa staa huyo bado yupo Msimbazi. "Uongozi umemwomba Kocha Roberto Oliviera 'Robertinho' kukaa na staa huyo ili wamalizane vizuri kama...

1 day ago


Mwanaspoti Sports
Simba yafuata beki Muivory Coast

SIMBA imeamua kuboresha kila idara kwenye kikosi chake, achana na winga Kramo Aubin inayoweza kumalizana naye muda wowote, sasa imetua kwa beki wa kati Coulibaly Wanlo raia wa Ivory Coast kutoka ASEC Mimoses. Taarifa zilizoandikwa juzi Jumatatu na Mwanaspoti, zilieleza jinsi Simba ilipofikia mazungumzo na winga Aubin, lakini baada ya kuona kuna beki mahiri, ikaamua kupiga ndege wawili kwa jiwe moja kwa kuanza kufanya naye mazungumzo. Chanzo cha taarifa hizo kinasema: "Lengo lilikuwa ni winga, lakini mtathimini wetu wa viwango...

1 day ago


Milard Ayo General
Maneno ya Ahmed Asas katika kuadhimisha siku ya Maziwa Duniani June, 1, 2023

Ni June 1, 2023 ambapo sehemu mbambali inaadhimisha siku ya Maziwa Duniani. Sasa hapa tunae Mkurugenzi wa kampuni ya Asas inayohusika kusambaa na uuzaji wa Maziwa Tanzania, Ahmed ambae ametuma salamu kwa watanzania hususani katika siku hii ya leo ya maadhimisho hayo. “Kuna umuhimu sana wa unywaji wa maziwa kwa watu kwani kitaalamu kwa mujibu

1 day ago


Milard Ayo General
Kenya yasherehekea Siku ya Madaraka,kufanyika nje ya Nairobi tangu Rais William Ruto achukue madaraka.

Sikukuu ya Madaraka ya mwaka 2023 ni sherehe ya kitaifa ya kwanza kufanyika nje ya Nairobi tangu Rais William Ruto achukue madaraka. Sikukuu ya Madaraka inasherehekewa na wakenya kama ukumbusho wa wakati ambao nchi yao ilipata madaraka mnamo wa mwaka wa 1963 kutoka kwa waingereza na husherehekewa kila tarehe 1 mwezi wa sita kila mwaka

1 day ago


Taifa Leo General
Maporomoko yaua wanaume wawili wakilala pangoni Mama Ngina

NA WACHIRA MWANGI WANAUME wawili wameaga dunia kutokana na majeraha waliyopata huku mmoja akipigania maisha yake baada ya maporomoko ya ardhi kutokea karibu na kivuko cha Likoni, kwenye Kisiwa cha Mombasa leo Alhamisi asubuhi. Watatu hao walikuwa wamelala katika mojawapo ya mapango yaliyo kando ya eneo la Mama Ngina Waterfront wakati udongo uliporomoka na kuwaua

1 day ago


Taifa Leo General
Mzee arushwa jela kwa ulaghai wa shamba

Na RICHARD MUNGUTI MZEE wa miaka 60 atakula maharagwe kwa miaka mitatu gerezani baada ya kupatikana na hatia ya ulaghai wa shamba mjini Nanyuki, Laikipia miaka minne iliyopita. Gabriel Njoroge Mbuthia alifungwa na hakimu mwandamizi mahakama ya Milimani Bw Bernard Ochoi. Bw Ochoi aliyempata na hatia Mbuthia ya kughushi cheti cha umiliki wa shamba la

1 day ago


Milard Ayo General
Amazon kulipa zaidi ya bil.70 kwa madai ya upelelezi wa siri kwa wateja

Amazon imekubali kulipa $30.8m ili kutatua madai kwamba ilikiuka faragha ya wateja, ikiwa ni pamoja na kupeleleza wanawake katika nyumba zao. Kampuni hiyo kubwa ya teknolojia ilikubali kulipa $5.8m  sawa na zaidi ya Tsh. bil 70 baada ya Tume ya Biashara ya Shirikisho la Marekani (FTC) kusema mfanyakazi wa zamani wa Amazon alikuwa akiwapeleleza wateja

1 day ago


Taifa Leo General
Ntalami aomboleza kifo cha mbwa wake

NA MERCY KOSKEI MJASIRIMALI na mwanzilishi wa Marini Naturals, Bi Michelle Ntalami, anaomboleza kifo cha mbwa wake. Mbwa huyo kwa jina Pixel, anadai alifariki kwa njia tatanishi. Katika ujumbe mzito wa tanzia kwenye akaunti yake ya Instagram, Jumatano, Mei 31, 2023, Ntalami alieleza huzuni yake na kumtaja Pixel kama “mtoto” wake ambaye walikuwa na uhusiano

1 day ago


 Job Vacancy Highlights Show All 
Milard Ayo General
Baraza la Wawakilishi la Marekani linapiga kura ya ‘ndiyo’ kuhusu mpango wa kikomo cha deni

Baraza la Wawakilishi la Marekani limepiga kura kuendeleza mswada wa pande mbili ili kuongeza ukomo wa deni, ambao unaweka kikomo cha pesa ambazo serikali ya shirikisho inaweza kukopa. Baada ya kuitisha kura iliyorekodiwa, Bunge lilipitisha mswada huo 314-117 katika kikao cha usiku wa manane siku ya Jumatano. Katika kura hiyo ya Jumatano, wabunge 314 walipitisha

2 days ago


Taifa Leo General
Erick Omondi na Amber Ray kuporomosha kibao pamoja

NA MERCY KOSKEI MCHESHI Erick Omondi na mwanasosholaiti Amber Ray wametangaza kuwa wamejitosa kwenye muziki huku wakitarajia kutoa wimbo wao wa kwanza Ijumaa, Juni 2, 2023. Kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii, wawili hao walipeana habari hizo za kusisimua, huku Amber Ray akijitambulisha kama rapa mpya zaidi mjini, na kusema kuwa tofauti yake na wasani wengine

2 days ago


US to resume Sudan mediation once parties 'serious'

The United States said there had been "serious violations of the ceasefire by both sides".

2 days ago


Taifa Leo General
Kamene na Bonez washangaza wakidai hutumia mswaki mmoja  

  NA MERCY KOSKEI ALIYEKUWA mtangazaji wa Kiss FM, Kamene Goro na mpenzi wake DJ Bonez wamewaacha wanamitandao kwa mshangao baada ya kufichua kuwa wanatumia mswaki moja. Mtangazaji huyo wa zamani katika mchezo wa kuulizana maswali kwenye akaunti yake ya Instargam ‘How well do you know your partner‘ alifichua kuwa wanatumia mswaki mmoja na mumewe, jambo ambalo

2 days ago


Taifa Leo General
Utata wa kesi ya mvulana wa miaka 13 akinajisi msichana wa miaka 4  

  NA TITUS OMINDE MVULANA wa miaka 13 anayekabiliwa na mashtaka ya unajisi kinyume na sheria ya makosa ya ngono ya 2006 atajua hatima yake Juni 6, 2023 baada ya mahakama ya Eldoret kuahirisha kesi yake. Mnamo Jumatano, Mei 31, 2023 hakimu mwandamizi wa Eldoret Caroline Waltima aliahirisha kusomewa mashtaka akisubiri kuteuliwa kwa wakili wa

2 days ago


Taifa Leo General
Vituko: Sonko athibitisha ‘blingi’ zake si feki

Na MWANDISHI WETU ALIYEKUWA gavana wa Nairobi Mike Sonko alithibitisha kuwa blingi (vito) anavyovaa vya dhahabu si ghushi. Kwenye video aliyoposti mtandaoni, Sonko alimsuta mwakilishi wa wadi ya Kileleshwa Robert Alai kwa kueneza uvumi kuwa vito vyake ni feki. Alai na Sonko wamekuwa wakivutana mtandaoni kuhusu uhalali wa vito anavyovaa Sonko huku wakisutana kwa maneno

2 days ago


EAC extends regional force mandate to September

EACRF's future had been uncertain since its mandate expired in March.

2 days ago


Taifa Leo General
Madaraka Dei 2023: Rangi maridadi za vikosi vya pamoja vya usalama gwarideni

  NA SAMMY WAWERU RAIS William Ruto anaongoza taifa Alhamisi kuadhimisha Madaraka Dei, Juni 1, 2023.   Ni siku Kuu ambapo Kenya huiadhimisha kila mwaka, kukumbuka siku ambayo ilipata uhuru wa ndani kwa ndani kujitawala kutoka kwa serikali ya Mbeberu 1963. Maadhimisho haya yanafanyika katika Uwanja wa Moi, Kaunti ya Embu. Vikosi vya pamoja vya

2 days ago


Milard Ayo General
Habari kubwa Magazetini Kenya leo June 1, 2023

Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania June 1, 2023,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma Magazetini kenya.

2 days ago


Taifa Leo General
Moraa aamua kushiriki riadha za polisi badala ya Diamond League nchini Italia na Ufaransa

Na AYUMBA AYODI BINGWA wa Jumuiya ya Madola mbio za mita 800, Mary Moraa amejiondoa kutoka duru za riadha za Diamond League za Florence (Italia) na Paris (Ufaransa). Moraa, ambaye alifaa kutimka mbio za 400m mjini Florence mnamo Juni 2 na mbio za 800m jijini Paris mnamo Juni 9, sasa ameelekeza nguvu zake katika riadha

2 days ago


Taifa Leo General
Mchango wa Shakahola kwa vita vya uhuru wa Kenya

NA MAUREEN ONGALA WAKATI Kenya inasherehekea sikukuu ya Madaraka Dei, jamii ya Wamijikenda inaendelea kukumbuka mchango wa msitu wa Shakahola kwa vita vya ukombozi wa nchi kutoka kwa wakoloni. Msitu huo ulio katika eneobunge la Magarini, Kaunti ya Kilifi, kwa miezi kadha sasa umezoa sifa mbaya ya mauaji ya halaiki ya watu wanaoaminika walikuwa waumini

2 days ago


Taifa Leo General
Madaraka Dei Juni 1, 2023

NA SAMMY WAWERU RAIS William Ruto Alhamisi, Juni 1, 2023 ataongoza taifa kuadhimisha Sikukuu ya Madaraka Dei 2023. Ni siku maalum inayoadhimishwa Juni 1 kila mwaka kusherehekea uhuru wa ndani kwa ndani Kenya kujitawala, kutoka kwa serikali ya Mbeberu. Maadhimisho ya 2023 yananyika katika Uwanja wa Moi, Embu. Wananchi kutoka sehemu mbalimbali za nchi, walianza kufurika

2 days ago


Mtanzania General
IWPG, Wanahabari wahimiza amani

Na Mwandihi Wetu, Mtanzania Digital Wanahabari mbalimbali kutoka nchi za Ethiopia, Tanzania, Misri na Saudi Arabia wamekutanishwa katika jukwaa la mtandao na kujadili kuhusu umuhimu wa kudumisha amani dunianai. Mkutano huo uliofanyika juzi, uliandaliwa na Shirika la kimataifa lilijikita katika kuhamasiha amani la IWPG lenye hadhi Maalum ya Ushauriano ya Baraza la Umoja wa Mataifa

2 days ago


Milard Ayo General
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania leo June 1, 2023

Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Dar es salaam June 1, 2023,nakukaribisha kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma za Magazeti ya Tanzania,

2 days ago


Mtanzania General
Aliyedanganywa na shetani atupwa jela miaka 30 na viboko 12

*Ni baada ya kukiri kumbaka mtoto wa miaka 13 Na Malima Lubasha, Bunda MKAZI wa Mtaa wa Luselu katika mji wa Bunda mkoani Mara, Masubugu Masubugu (32) amehukumiwa kwenda jela miaka 30, kuchapwa viboko 12 na kulipa fidia Sh milioni moja baada ya kutiwa kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka 13 mwanafunzi wa shule

2 days ago


Taifa Leo General
Mzee wa jamii ya Boni adai hakuna cha kujivunia Madaraka Dei

NA KALUME KAZUNGU HUKU Kenya ikiadhimisha miaka 60 tangu kupata uhuru (Madaraka) kutoka kwa Mkoloni, mzee Badaa Abala,80, kwake hakuna cha kujivunia. Yeye ni mmoja wa Wakenya wanaotoka kwa jamii ya walio wachache ya Boni ambao makao au ngome yao kuu ni msitu wa Boni katika Kaunti ya Lamu. Akizungumza na Taifa Leo kijijini kwao

2 days ago


Mtanzania General
4 Most Successful African Teams in FIFA World Cup History

The FIFA World Cup is one of the most celebrated football tournaments globally. Attracting millions across the globe, the 2022 edition was fascinating as Argentina trumped France in an exhilarating final. The world cup also presents opportunities for punters to stake on international fixtures on top bookmakers like SportingBet and get attractive bonuses as detailed

2 days ago


Taifa Leo General
Rais Ruto awateua makatibu wawili wa wizara kujaza nafasi zilizotokea

NA CHARLES WASONGA  RAIS William Ruto mnamo Mei 31, 2023 amependekeza watu wawili wapya kwa uteuzi kuwa Makatibu wa Wizara. Bi Salome Wairimu Muhia-Beacco ameteuliwa kuwa Katibu wa Idara ya Magereza katika Wizara ya Usalama wa Ndani, kuchukua pahala pa Esther Ngero aliyejiuzulu juzi. Bi Muhia-Beacco ni Wakili wa Mahakama Kuu mwenye tajriba ya miaka

2 days ago


Taifa Leo General
Shakahola: Awamu ya pili ya upasuaji maiti yakamilika katika mochari ya Malindi

NA ALEX KALAMA WATAALAMU wa upasuaji wa maiti wametamatisha awamu ya pili ya upasuaji wa maiti za Shakahola mnamo Jumatano katika mochari ya Hospitali Kuu ya Malindi. Jumla ya miili 16 imefanyiwa uchunguzi. Akizungumza baada ya kukamilisha shughuli hiyo, mwanapatholojia mkuu wa serikali Dkt Johansen Oduor ameeleza kuwa yule mtu aliyefariki katika hospitali ya Malindi

2 days ago


Wasomi Ajira General
NBA Finals 2023 – Everything you Need to Know

NBA Finals 2023 – Everything you Need to Know , How many games are in the NBA Finals? , How many times has Jimmy Butler been to the Finals? , How many 8 seeds have made it to The NBA Finals? ,How many times have the Heat been to the Finals? NBA Finals 2023 –

2 days ago


Taifa Leo General
Washukiwa wa uvamizi wa shamba la familia ya Kenyatta kufikishwa mahakamani

NA CHARLES WASONGA WAZIRI wa Usalama wa Ndani Profesa Kithure Kindiki mnamo Jumatano, Mei 31, 2023 ametangaza kuwa washukiwa kadha watafikishwa mahakamani kuhusiana na uvamizi uliofanyika katika shamba la familia ya Rais mstaafu Uhuru Kenyatta mapema mwaka huu katika eneo la Ruiru, Kaunti ya Kiambu. Kwenye kikao na wanahabari nje ya afisi yake iliyoko Jumba

2 days ago


Milard Ayo General
Rafiki wa MC aliyejirusha ghorofani atoweka, aacha ujumbe mzito (+video)

Ni siku 7 zimepita tangu Joel Misesemo (MC Joel) ajirushe kutoka ghorofa 7 Makumbusho DSM. Leo AyoTV imepata taarifa juu ya Rafiki wa karibu wa MC JOEL, aitwaye Tyson Nduguru nae ametoweka anatafutwa na Familia yake. Maswali yaliyozua mjadala ni Inakuwaje rafiki yake ajirushe ghorofani May 23,2023, nae apotee May 26, 2023 akiwa ameaga anaenda

2 days ago


Milard Ayo General
Bilioni 4 zimetengwa kwa Wabunifu, watapewa Milioni 50+ watakaokidhi vigezo

UNDP Tanzania, kupitia proramu yake ya FUNGUO, imefungua dirisha la pili la udhamini kwa kampuni changa za kibunifu za Kitanzania. FUNGUO inayofadhiliwa na Umoja wa Ulaya pamoja na Serekali ya Uingereza, imetangaza kutoa ufadhili wenye thamani ya shilingi bilioni moja ili kuchangia katika uchumi na maendeleo ya nchi kwa ujumla. Kwa kuzingatia jitihada za makusudi

2 days ago


Milard Ayo General
Isaac anayedaiwa kumng’oa Jino mke wake afikishwa Mahakamani, anyimwa Dhamana

Isaac Mnyagi mkazi wa kata ya Sombetini Katika jiji la Arusha amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Arusha amesomewa shtaka la shamulio la kumdhuru mwili wa mke wake Jackline Mkonyi kwa kumpiga sehemu mbalimbali za mwili wake pamoja nakumg’oa jino kwa kutumia ‘plaiz’ Mbele ya Hakimu,Jenifa Edward wa mahakama ya wilaya ya Arusha,katika kesi namba

2 days ago


Mtanzania General
RC Pwani ahimiza watendaji kutumia takiwmu za Sensa kwa maendeleo

Na Gustafu Haule,Pwani MKUU wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, amewaagiza watendaji waliopo katika Halmashauri pamoja na wataalamu mbalimbali kutumia takwimu za Sensa ya mwaka 2022 katika kuendeleza shughuli za kiuchumi na maendeleo zinazofanyika Mkoani humu. Kunenge, ametoa kauli hiyo leo Mei 31, wakati akifungua mkutano wa mafunzo ya matumizi ya matokeo ya kwa kamati za 

2 days ago


Mtanzania General
Waziri Tax afanya mazungumzo na Balozi wa Urusi

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Stergomena Tax (Mb.) amekutana kwa mazungumzo na Balozi wa Shirikisho la Urusi nchini, Andrey Avetisyan katika ofisi za Wizara Jijini Dododma leo Mei 31, 2023. Katika mazungumzo hayo, viongozi hao wamekubaliana kuimarisha ushirikiano wa kihistoria na kidiplomasia uliopo baina

2 days ago


Mtanzania General
Dk. Gwajima azindua programu ya Jinsia ANAWEZA

*Kuwezesha Wanawake kiuchumi Na Mwandishi Wetu, Dodoma Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dk. Dorothy Gwajima amezindua Programu ya Jinsia ya ANAWEZA itakayowawezesha wanawake kiuchumi na kushiriki katika nafasi mbalimbali za uongozi kwa niaba ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Philip Mpango leo Mei 31, 2023.

2 days ago


Milard Ayo General
Katibu wa CCM Daniel Chongolo atoa siku 10 kwa Waziri wa Maji kukamilisha mradi wa maji katika Wilaya ya Kilolo

Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo ametoa siku 10 kwa Waziri wa Maji Jumaa Aweso kufika katika mradi wa maji katika kata ya Uhambingeto Wilaya ya Kilolo kusimama kwa zaidi ya miezi sita na kusababisha wananchi wa kata hiyo kutopata huduma ya maji ambapo walitakiwa kupata tangu mwezi wa tatu mwaka huu. Ametoa maagizo hayo

2 days ago


Taifa Leo General
Azimio wazima mazungumzo ya maridhiano hadi wakati usiojulikana

NA CHARLES WASONGA HATIMAYE muungano wa Azimio la Umoja-One Kenya umetangaza kuwa mazungumzo ya maridhiano kati yake na Kenya Kwanza yameahirishwa hadi muda usiojulikana. Kwenye barua aliyomwandikia mwenyekiti mwenzake, George Murugara (Mbunge wa Tharaka) mnamo Jumatano, Mei 31, 2023, Otiende Amollo (Mbunge wa Rarieda) ambaye ni mwenyekiti wa wawakilishi wa Azimio katika mazungumzo hayo, amesema

2 days ago


Mbosso 3 weeks ago  
Nandy - The African Princess 2 weeks ago  
MariooOfficial 2 weeks ago  
MariooOfficial 3 weeks ago  
Zuchu 1 month ago  
Alikiba 2 weeks ago  
Anjella 23 hours ago  
Yammi 1 week ago  
Walter Chilambo 1 day ago  
Rayvanny 3 weeks ago  
Chudy love 4 weeks ago  
Martha Mwaipaja 2 weeks ago  
kontawa 1 month ago  
Harmonize 1 week ago  
Mwanaspoti Sports
HISIA ZANGU: Wananchi walivyoloa ndani na nje ya uwanja Lupaso

ILIANZA kuwa siku mbaya kisoka kwa Wananchi pale walipoamka na mvua usiku wa kuamkia juzi. Ikaenda kuwa siku mbaya wakati shabiki wao mmoja alipokata kauli wakati akigombea kuingia uwanjani katika kile kinachoitwa kugombea kuingia uwanjani bure. Nashauri tuachane na soka la bure. Siku ikawa mbaya wakati wachezaji wa pande zote mbili, Yanga na USMA Alger waliposhindwa kuonyesha uhodari wao katika uwanja uliojaa utelezi. Mpaka leo wanatuachia swali, hali ingekuaje kama uwanja ungekuwa katika ubora wake? Hatuwezi kujua. Vyovyote ilivyo, kwa...

2 days ago


Milard Ayo General
Rais Mwinyi azindua kamati ya maridhiano

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi awashukuru Viongozi wa Chama cha ACT Wazalendo kwa kukubali kukaa pamoja na Viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM ili kuendeleza dhamira ya kushirikiana na kuimarisha Umoja wa Kitaifa Zanzibar. Ameyasema hayo leo alipozindua Kamati ya maridhiano kati ya CCM na ACT Wazalendo Ikulu,

2 days ago


Zimbabwe general election set for August 23

If an election run-off for president is necessary, it will be held on October 2.

2 days ago


Taifa Leo General
Serikali yakubali tope la Shakahola

MARY WAMBUI Na ALEX AMANI SERIKALI imekubali kubeba lawama kwa kushindwa kuzuia kutokea kwa vifo vya watu kwenye msitu wa Shakahola. Waziri wa Usalama wa Ndani Prof Kithure Kindiki akihutubia wanahabari jijini Nairobi leo Jumatano amesema kulikuwa na utepetevu na maafisa wa usalama walizembea wakashindwa ‘kugundua’ na kuzuia maafa ya wanaoaminika kuwa walikuwa wafuasi wa mhubiri

2 days ago


Mwanaspoti Sports
Geay apata Sh200 milioni kwa saa mbili

JANA, tuliishia sehemu ambayo Geay anazungumza kuhusu mbio za Boston ambazo zimempa umaarufu mkubwa, leo anaendelea kuzungumza kuhusu mbio hizo, na bei ya kiatu alichovaa siku hiyo. KUHUSU FEDHA ALIZOPATA KWENYE BOSTON “Mara nyingi fedha kwenye mashindano haya zinaonekana, mimi nilipata kiwango cha fedha, siyo kikubwa lakini kwangu siyo kidogo kwani nilipata nafikiri milioni 150, ukichanganya na bonasi na fedha nyingine za mikataba, ilifika milioni 200, kumbuka hii ni kwa saa mbili tu ambazo nilikimbia pale. “Hiki kwangu ndiyo kiwango...

2 days ago


Milard Ayo General
Wabunge washauri Songas kuongezwa mkataba kwa ufanisi wa kazi

Mbunge wa Jimbo la Singida Magharibi Elibariki Kingu amekuwa miongoni mwa wabunge waliochangia makadirio ya mapato na matumizi ya wizara ya Nishati kwa mwaka wa Fedha 2023/24.

2 days ago


Mwanaspoti Sports
Yanga ilinasa kwenye mtego wa Waarabu

KABLA ya mchezo wa kwanza wa fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika juzi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa dhidi ya Yanga, USM Alger haikuwa na takwimu za kuvutia katika umiliki wa mpira na kucheza soka la pasi. Lakini pia USM Alger ilikuwa na takwimu bora za ulinzi licha ya kwamba ilikuwa imeruhusu idadi kubwa ya mabao kuliko Yanga kwenye mashindano hayo hasa katika uporaji wa mipira, uzuiaji mashuti na kuziba mianya kwa wapinzani. Inawezekana Yanga walizifahamu takwimu hizo hawakuamua kuzipa...

2 days ago


Mtanzania General
Wizara ya Nishati yaomba Trilioni 3.04

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital Waziri wa Nishati, January Makamba ameliomba Bunge kuidhinisha Sh Trilioni 3.04 kwa ajili ya kwa ajili ya matumizi ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake kwa Mwaka wa Fedha 2023/2024. Waziri Makamba ametoa hoja hiyo leo Mei 31, 2023 bungeni jijini Dodoma ambapo amesema Sh trilioni 2.96 sawa na asilimia

2 days ago


Taifa Leo General
Waliovamia shamba la familia ya Uhuru Kenyatta kukamatwa

NA SAMMY WAWERU MSAKO wa wahuni waliovamia shamba la familia ya Rais mstaafu Uhuru Kenyatta Machi 2023, unatarajiwa kuanza hivi karibuni. Akihutubia taifa kuhusu hali ya usalama nchini, Waziri wa Usalama wa Ndani Prof Kithure Kindiki alisema Jumatano, Mei 31, 2023 kwamba uvamizi wa shamba la rais huyo mstaafu ni hatia inayohitaji adhabu kali. “Uvamizi

2 days ago